*HATUA KWA HATUA MALEZI YA VIFARANGA*
Na *Comrade Ally Maftah*
0762212623
*Kwa Kifupi Sana fanya yafuatayo utanishukuru*
Kwanza kabisa vifaranga wanahitaji Sana Mambo yafuatayo yazingatiwe.

Joto

Chakula Safi

Maji Safi

Mzunguko mzuri wa hewa

Idadi sahihi ya Vyombo vya chakula na Maji

Randa Safi ,zisizo na vumbi, kavu

Biosecurity/ usalama wa viumbe.
NISEME TU KWAMBA FUATA HAYA KWA VITENDO KABISA UTAFAULU

*WIKI LA KWANZA*

Siku ya kwanza kabisa ( Glucose/Glucovet inategemea wametoka umbali gani wanaweza kupewa masaa 3-24).

*Multivitamins* Mfn! Neoxychick, Chick formula ,Tetracovit Kwa siku ya kwanza Hadi ya 3-5.

Siku ya 6 huwa tunashauri wapewe maji tupu,

Siku ya Saba ni chanjo ya kwanza ya NEWCASTLE/ KIDERI-MDONDO

Muda huu wote watakua wanatumia chakula cha Starter/ Broiler starter.

Siku ya nane Hadi siku ya 12 Wapewe vitamins zipo Aina nyingi Sana *Mfn* :Aminototo, Introvit Farmvita, Dad OCTAVIT, etc

Siku ya 13 wapewe maji matupu ( japo hata ukiwawekea vitamins si mbaya).

Siku ya 14 wapewe chanjo ya Pili ya Infections Bursal Disease / Gumboro

Muda huu wote wapewe chakula cha Starter/ Broiler Starter.

Hapa tuna wagawa kuku kutokana na Aina

*KUKU WA NYAMA/BROILERS*

Siku ya 14 au15 Hadi ya 22 wapewe Grower Pellets ( Kwa uzoefu wangu).

Hapa hawa kuku wanaweza kupewa Vitamins au Broiler Booster Mfn : Introvit A , Galvet am aUtravin broiler booster.

Siku ya 21 kuku Broiler wapewe chanjo moja wapo Kati ya Gumboro au KIDERI ( Hii inategemea MAZOEA ya namna ya kuchanja kuku kutokana na mkoa ulipo).

*_KWA KUKU WANAOANDALIWAKUTAGA ( CHOTARA, LAYERS , KUKU WA KIENYEJI)._*

Wapewe chakula cha Starter Mashi inaenda mpaka wiki ya 7 au wiki ya 8 (inategemea maelezo ya chakula unachotumia na kampuni uliyo nunua chakula).

Siku ya 21 kuku hawa watapewa Chanjo ya pili ya Newcastle/KIDERI/MDONDO

Siku ya 28 kuku wanao andaliwa kutaga wa
Comments
Post a Comment