*MFANO WA KUANDAA MRADI WA KUKU WA MAYAI 500.* Na Comrade Ally Maftah www.camstore.co.tz Mfano Wa Mpango Wa Biashara Wa Kuku Wa Mayai 500... Mjasiriamali mfugaji, Uzalishaji wa mayai ni biashara ambayo huleta faida kubwa sana kwa wajasiriamali wafugaji waliowekeza mitaji yao katika sekta hii. Changamoto ya wengi wao hufanya biashara ya ufugaji bila ya kuwa na mwongozo wa mpango wa biashara. Pata mfano hapa jinsi ya kuandaa mpango wa biashara wa kurasa 1 wa kuku wa mayai wa kibiashara 500.
MAONO Kuwa shamba linaloongoza kwa kuzalisha bidhaa salama za ufugaji wa kuku hapa Tanzania.
MISHENI Kuzalisha mayai bora kwa kutumia njia za kisasa za ufugaji wa kibiashara wa kuku wa mayai.
MALENGO ya muda mfupi ni kuzalisha mayai bora 460 kila siku kwa kutumia lishe bora ilio salama na nafuu toka hapo shambani.
MALENGO ya muda mrefu ni kusambaza mayai bora mwaka hadi mwaka kwa kuwa na bachi tatu za kuku 500 zinazo tofautiana kwa wiki 21.
BIDHAA Kuuza mayai, mbolea, manyoya, shamba darasa, kuku waliochoka kutaga, nk.
KUJITOFAUTISHA Kuwapatia wateja walengwa mayai yaliyo bora na kwa bei nafuu sana sokoni.
MPANGO WA MASOKO Kujitangaza katika maeneo ya jirani na mtandao wa Instagram kwa wateja walengwa ambao ni migahawa na wauza chipsi.
MAHITAJI Mabanda ya kuku, bruda, vyombo vya chakula na maji, chakula cha kuku, chanjo, maji, umeme, nk.
MFANYAKAZI Mjasiriamali, mhudumu, muuzaji wa mayai, mhasibu, mlinzi, nk.
MPANGO WA FEDHA Makadirio ya mtaji unaohitajika kuanzisha mradi wa kuku wa mayai wa kibiashra 500 Tshs 10m.
Mjasiriamali mfugaji kabla ya kuanza ujasiriamali wa ufugaji kuku, zingatia kuandaa mpango wa biashara kwa ajili ya kukuongoza na kutimiza malengo yako kwa mafanikio.
KWA USHAURI ZAIDI
■CALL
0762212623
0712163738
*CAMSTORE IPO KWA AJILI YAKO

Comments
Post a Comment